Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Professor Jay amefunguka na kusema kuwa bifu zinazoendelea kwa wasanii zinaweza kutokea bifu kama za Tupac na BIG.

Professor Jay amesema kuwa kina Tupac na BIG walianzia huku, ikaenda mashabiki wanakuwa viherehere hawana mpango, wanayumba kama dera.

Pia amesema kuwa Ndio maana kila linalosemwa, miziki yote na mambo ya ajabu ajabu yana Trend, ni Trend za kishamba sana zinazoenda kuharibu muziki wetu.

Sasa baadaye wataanza kuleteana bifu mtaani (uso kwa uso inakuwaje), sisi tutakuwepo, mimi nasema sasa hivi halafu baadaye nitanyamaza kimya nasitataka mtu aniambie niseme.”

“Sisi tumepitia hii game muda mrefu sana, Tupac anakufa tunajua amekufaje, Biggie amekufa tunajua amekufaje.

Hii sanaa ya bongo inavyoenda, maana wanaambiana vya ndani. Wameingia kwenye bifu, athari zake zinajulikana hata kwa mashabiki sio nzuri.

Hii game naisema naiangalia huko chini ikoje, na kule ndio kuna mashabiki wengi sio hao washua wamevaa tai wanacheka cheka tu kule chini kuna shida. Kesho na kesho kutwa wasanii chipukizi nao itabidi watengeneze bifu mara mbili yake ili wapande kama wao wanavyofanya.”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *