Mwanamuziki wa Hip Hop Bongo, Joh Makini ametajwa kuwania tuzo za Hip Hop nchini Uganda maarufu kama; MTN Uganda Hip Hop Awards, ambazo zimepangwa kufanyika Mei 16, 2021.
Joh Makini ametajwa kuwania kipengele cha Msanii Bora wa Mwaka – Afrika Mashariki kupitia wimbo wake ‘Dangerous’ aliyomshirikisha Nahreal.
Kwenye kipengele hicho Joh Makini anachuana na wasanii kama Khaligraph Jones, Nyashinski, Femi One na King Kaka wote kutoka Kenya.
Kipengele kingine ambacho Mwamba ametajwa kuwania ni Kolabo Bora ya Mwaka kupitia wimbo ‘Abaana Beeka’ alioshirikishwa na rapa Navio wa Uganda.
Tuzo hizo za Hip Hop zinatarajia kufanyika Mei 16 mwaka huu nchini Uganda ambapo wasanii mbali mbali watawania tuzo hizo.