Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Rayvanny amehojiwa katika kituo polisi kanda maalum Dar es Salaam kwa saa sita kutokana na kusambaza picha za utupu kuhusu Harmonize.
Rayvanny alifika kituoni hapo saa tatu asubuhi na kuwa katika mahojiano na maofisa upelelezi.
Rayvanny aliyekuwa amevalia shati la drafti ya rangi bluu na nyeusi na suruali nyeusi alitoka ndani ya kituo hicho akiwa na wanaume wawili.
Alipomaliza kushuka ngazi za kituoni hapo walinzi wake waliokuwa wakimsubiri kwa nje walimfuta na kuongozana nao hadi kwenye gari ya rangi nyeusi aina yaTX Prado lililokuwa limeegeshwa nje ya geti la kituo hicho.
Hata hivyo sio yeye wala watu aliokuwa nao, hakuzungumza chochote na waandishi waliokuwepo eneo hilo.
Katika hatua nyingine hatua chache toka kwenye geti hilo,alikuta wanafunzi wakimshangalia na kufuata gari lake barabarani hali iliyomlazimu kufungua vioo na kuanza kusalimiana naye kwa muda wa dakika tatu kabla hajaondoka eneo hilo.