Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Baba Levo amefunguka na kuthibitisha kuwa ameitwa na baraza la Sanaa la taifa kutokana na kinachoendelea mtandaoni.

Baba Levo amethibitisha hayo kupitia akaunti yake ya Instagram “Ni kili Kupokea Simu Ya Mtu Aliyejitambulisha kutoka Balaza La Sanaa..! Na Kunitaka Nifike Kesho Saa Tano Asubuhi Ofisini Kwao.

Pia ameendelea kuandika kuwa Kuanzia Saa Tatu Asubuh Ntakuwa Pale ili Kuepuka Foleni..!! LINK KWENYE BIO”.

Wito wa Basata kwa Baba Levo unatokana na mambo yanayoendelea katika mitandao ya kijamii baada ya kumshambulia vikali mwanamuziki Harmonize.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *