Mwanamuziki a Bongo Fleva, Juma Jux amelamba dili la kusambaziwa bidhaa zake kama Kofia, T-Shirts na viatu kupitia brand yake ya African Boy.
Kupitia kwenye ukurasa wake wa Instagram Jux ameandika “Unapofanya kazi kwa bidii, na ukaweka malengo huku ukimtanguliza Mungu, lazima utaona mafanikio ya kazi yako. Wakati naanzisha brand ya African Brand tulianza kwa speed ya kutambaa kabisa, tukawa tunatengeneza t-shirts kadhaa tu, tunavaa na kuuza.
Pia amendika Baadae nilipo kwenda China kimasomo nikapata wazo la kukua zaidi, tukaanza kujiongeza, team ikaanza kuongezeka, tukaongeza bidhaa kutoka T-shirts peke yake hadi kuwa na Raba, kofia, boxer, Hood, body spray na cover za simu.
Kutoka kutengeneza t-shirts zetu hapa Kariakoo na kuziuza kwa washkaji, hadi kufikia level ya brand yetu kupatikana nchi kama za Tanzania, Kenya, Uganda, Congo, Sudan, South Africa, Marekani.
Najivunia sana leo kuwajulisha ukubwa huu tulioufikia hadi kufanikiwa kusaini mikataba ya usambazaji ili kutanua wigo wa kimataifa zaidi. Ningeweza kukata tamaa kipindi cha nyuma na kuamua kuwa balozi wa brand yoyote ya mavazi, lakini ndoto yangu ya kuweza kuwa na brand ya mavazi ya kitanzania inayovaliwa ulimwenguni ilinisukuma kuweza kuendelea hadi kuweza kufika walau hatua hii.
Ningependa kuwashukuru sana mashabiki zangu, familia yangu, ndugu, jamaa, marafiki na management yangu. Namshukuru Mungu pia kwa hatua hii, ni hatua kubwa lakini safari ndiyo kwanza inaanza.
Pamoja na kulamba dili hilo Jux hajaweka wazi jina la kampuni aliyoingia nayo mkataba wa usambazaji wa bidhaa zake hizo.