Msanii wa Bongo Fleva, Amber Lulu ametupa jiwe gizani kuhusu wanawake wanaoweka mapenzi yao hadharani kwa upande wa Instagram na kuwatag wapenzi wao ambao baadae wanaishia kuwasaliti.
Kupitia Instastory yake ameandika ni jinsi gani anawashangaa wanawake wanaowatangaza wapenzi wao Instagram huku wakiwatag ila baada ya wapenzi wao kupata meseji kadhaa wanaanza kubadilika,baada ya wapenzi wao kubadilika waanza kutafuta mchawi nani.
Inasemekana Amber Lulu ametupa dogo kwa mmoja kati ya marafiki zake,je ni nani anaetupiwa dongo hili kutoka kwa Amber Lulu.
Msanii huyo kwasasa amefanikiwa kupata mtoto ambaye amejifungua mapema mwaka huu na kumfanya aitwe mama kutokana na mtoto huyo.