Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Gigy Money amefunguka na kusema kuwa anatamani afunguliwe na afanye kazi zake za muziki kama ilivyokuwa zamani kabla ya kufungiwa.
Baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuagiza kufunguliwa kwa vyombo mbalimbali vya habari vilivyofungiwa Gigy Money naye anatamani kufunguliwa.
Rais Samia leo Jumatatu Aprili 6, akiwa anawaapisha makatibu wakuu, naibu makatibu wakuu wa wizara na wakuu wa taasisi mbalimbali katika moja ya mambo aliyoyazungumzia ni kuagiza kufunguliwa kwa vyombo vya habari vilivyofungiwa lakini vifuate sheria .
IBaada ya agizo hilo@gigy_money_og alipost picha kupitia ukurasa wake ukurasa wake wa Instagram ana kuandika Sijui Na mimi nitafunguliwa.
Januari 5, 2021, Baraza la Sanaa Tanzania, (Basata) ilitangaza kumfungia miezi sita msanii huyo kutojihusisha na kazi za sanaa ndani na nje ya nchi.
Basata ilisema ilifikia hatua hiyo baada ya Gigy akiwa katika tamasha la ‘Tumewasha Tour’, jijini Dodoma kuwa na vazi lililoonyesha maungo yake ya mwili.
Walibainisha kuwa kitendo hicho kilidhalilisha utu wa msanii huyo na kubugudhi hadhira ya wapenda sanaa ndani na nje ya nchi.