Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Anjella kutoka Konde Gang amesema yeye bado ni mtoto mdogo sana ndio kwanza ana umri wa miaka 19 hivyo hataweza kuchanganya mapenzi na kazi kwa wakati mmoja kwani anahisi itamuharibia.
Anjella amesema kwa sasa yupo hayupo kwenye mahusiano kwa sababu wanaume wanahitaji uvumilivu pia yeye ni mtu wa dini hivyo anazingatia maadili na hawezi kujihusisha na mapenzi.
“Ni kweli sina mpenzi na sipo kwenye mahusiano, kwanza mimi ni binti mdogo nina miaka 19 hadi sasa”.
Pia amesema kuwa sitakiwi kujihusisha na hayo mambo siwezi ku-control mapenzi na kazi kwa wakati mmoja kwa hiyo itabidi nipige kazi na nilishaapa sitaki kuja kufa masikini hivyo lazima nipambane”.