Mwanamuziki wa Hip Hop Bongo, Young Killer ametangaza kusogeza mbele kuachia albamu yake mpya kupisha maombolezo ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
Msanii huyo ambaye jina lake halisi ni Erick Msodoki, ameyaeleza hayo kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa Instagram.
Mwaka jana msanii huyo alitangaza kuwa angeachia albamu yake Aprili 13, 2021 lakini kutokana na msiba wa taifa ameahirisha utoaji wa albam hiyo.
Kupitia ukurasa wake huo ameandika “Napenda kuwatangizia kuwa nimehairisha kutoka kwa albamu yangu kama nilivyoahidi mwaka jana kuwa albamu hiyo ingetoka tarehe 13 April 2021.
“Kufuatia msiba wa Kitaifa wa mpendwa wetu, Hayati John Magufuli ,natangaza kuwa albamu i yenye viwango vya juu kabisa, imesogezwa mbele mpaka hapo tarehe husika nyingine itakapo tangazwa.
Ameongeza “Najua wapenzi wa mziki wangu na mashibiki zangu mlingojea sana kwa hamu lakini najua kuwa nina watu wanao nipenda sana na wako tayari kuningojea.
Hivyo basi tutaanza kuachia project hivi karibuni na ninaahidi kuwafurahisha na kukata kiu yenu kwa kila kazi itakayotoka.