Mwanamuziki wa lebo ya High Table Entertainment, Elias Barnabas maarufu Barnaba Classic amefunguka kuwa moja ya changamoto kubwa ni kuendesha lebo na sio kufungua.

Staa huyo wa wimbo Tuachane Mdogomdogo alisema wasanii wengi wanadhani kuwa na lebo ni kuwa na jengo, studio na vifaa, lakini lebo ya muziki inahitaji zaidi ya vitu hivyo.

“Lebo ya muziki ni taasisi. Kila mtu anaweza kulipa pango akakodi nyumba, akanunua vifaa vya studio, lakini hiyo haihesabiki una lebo. Ugumu wa lebo uko kwenye kuitunza kuhakikisha inafanya kazi na inadumu, ndiyo maana lebo za wasanii wengi zinapoteaga tu,” alisema Barnaba.

Alijazia kuwa kwa sasa hata lebo yake ipo likizo ya kufanya kazi za wasanii na inatarajiwa kuanza rasmi wakati wowote.

“Lebo yangu haijafanya kazi kwa muda wa kama miezi sita sasa, lakini tunatarajia kurudi tena kazini mapema mwaka huu,” alisema msanii huyo ambaye ni zao la THT.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *