Muigizaji wa Bongo Movie, Jacqueline Wolper ambaye ni mjasiriamali mkubwa amechimba mkwara mzito kwa baadhi ya wanawake.
Wolper ametoa onyo kali kwa wale wanawawake wanaopenda kuchukua wanaume za watu huku wakijua ni wanaume za watu.
Wolper anasema kuwa mtu atakayemchukua mpenzi wake wa sasa ambaye ni mbunifu wa mavazi, Rich Mitindo watagawana majengo ya Serikali; mmoja apelekwe mochwari Muhimbili na na mwingine aende jela Segerea.
Amesema kuwa “Kwa kuwa niliamua mwenyewe kwa moyo wangu kuwa na Rich, sihitaji tena kuacha wala kuachwa na huyu.
Pia amesema kuwa Sasa hivi ni hama zangu ama zake kwa wanawake wanaojifanya wenyewe wapo mjini kwa ajili ya waume za watu; yaani tutabadlishana majengo ya Serikali,” anasema Wolper ambaye ni muuza vitenge maarufu jijini Dar es Salaam.