Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbas amesema wasanii ni miongoni mwa makundi maalum ambayo leo yatapata fursa ya kuuaga mwili wa Hayati Dkt. John Magufuli katika Uwanja wa Magufuli uliopo Chato.

Dkt. Abbas amesema wasanii hao hasa waliotunga nyimbo za maombolezo wataitumia fursa hiyo pia kuomboleza kwa kutumbuiza jukwaani nyimbo zao za maombolezo ikiwa ni nafasi yao kueleza jinsi marehemu alivyokuwa akithamini mchango wa sanaa nchini.

Kundi lingine litakalopata fursa ya kutoa heshima za mwisho ni waandishi wa habari, viongozi dini pamoja na wananchi wa Geita na mikoa ya jirani, shughuli itakayoanza saa 1 asubuhi ikiongozwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Aidha, Abbas amesema maziko rasmi yatafanyika Ijumaa Machi 26 nyumbani kwa Hayati Dkt. Magufuli, yakiongozwa na Rais Samia Suluhu huku Rais wa Uganda Yoweri Museveni akitarajiwa pia kuhudhuria.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *