Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Wastara Juma amefunguka na kusema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dk John Pombe Magufuli amegusa sana maisha yake.
Wastara alisema, Hayati Rais Magufuli ataendelea kuishi kwenye mioyo ya watu wengi kwani aliamua kujitoa sadaka kwa wengine na kwa upande wake, aliokoa maisha pale alipokuwa akisumbuliwa na tatizo la mgongo na mguu.
Amesema kuwa “Yani kwa kweli anashindwa hata namna ya kuelezea maana Rais Magufuli (hayati) alijitoa sana. Wewe angalia wakati ule mimi naumwa mguu na mgongo, aliona kwenye mtandao nilipoomba msaada na hapohapo alichukua hatua za haraka.
Pia amesema kuwa “Aliwatuma wasaidizi wake mpaka nyumbani kwangu Tabata na kuniletea shilingi milioni 15 cash ambazo walitoa yeye pamoja na mke wake mama Janeth.
Kwangu mimi wakati ule sikuwa na njia yoyote ya kupata hizo pesa maana zilikuwa zinahitajika na sikuwa nazo. Kwa kweli Mungu amlaze mahala pema peponi yule baba kwani alikuwa na moyo wa kipekee,”.
Msanii huyo alisema kuwa kutokana na maumivu ambayo anayo, ameamua kuingia studio na kumtungia wimbo pamoja na kurekodi video yake ambapo anaona angalau itampa ahueni ndani ya moyo wake.