Mama mzazi wa Diamond Platnumz, Bi Sandra maarufu kama Dangote amemjia juu msanii wa muziki Shilole baada ya kumpeleka shabiki wa kike kwa Diamond Platnumz muda mchache baada ya kumaliza mkutano wake na waandishi wa habari siku ya March 15,2021.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa Instagram Mama Dangote amechukizwa na kitendo hicho na kumsihi Shilole kutorudia tena kitendo kama hicho.

Mama Dangote ameandika “Kama mzazi hakuna anayefurahia kuona mwanae analetewa mwanamke ovyo ovyo bila kuzingatia staha ya mtu kama mtu, au imani zetu. Ukizingatia huyo mtu kashatangaza hadi pesa ili apige picha na mwanangu ila kwa kuwa tunajua nia yake ni ovu hatukumpa nafasi hiyo. mwanangu ni tafsiri halisi ya jamii( kioo cha jamii) yenye nidhamu tofauti na alivyo au ulivyomchukulia Shilole usirudie tena na siyo maisha kuchukuliana poa watu wakiwa kazini.

Pia ameandika kuwa hakuna msanii anayekubali kila mtu anayesema ni shabiki yake kirahisi..sisi ni wazoefu wa kushuhudia mashabiki ila siyo huyo au aina hiyo ya shabiki sijapenda Shilole ulichokifanya.

Kwa mujibu wa Shilole Shabiki huyo ametoka nchini Ufaransa na amefunga safari ili akutane tu na staa huyo wa muziki Barani Afrika na yeye alilifanikisha hilo kutokana na ukaribu uliopo kati yake na Diamond Platnumz.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *