Msanii nyota wa muziki kutokea Nigeria, Burna Boy ameshinda tuzo yake ya kwanza ya ‘Grammy’ kwenye kipengele cha ‘Best Global Music Album’ kupitia Album yake ya ‘Twice As Tall’ iliyotoka rasmi Agosti 14, 2020.

Burna Boy, ambaye jina lake halisi ni Damini Ogulu, alishinda tuzo hiyo kwenye utoaji wa tuzo ya Grammy ya 63, Machi 15 2021 uliofanyika mjini Los Angeles bila maudhulia kutokana na changamoto ya janga la Corona.

Burna anashinda tuzo hii ya Grammy kwa mara ya kwanza ikiwa ameshiriki kwa mwaka wa pili sasa.

Burna Boy anashinda tuzo hiyo kupitia ambum yake hiyo iliyowashirikisha wakali wengine wakiwemo Stormzy, Naughty By Nature, Chris Martin na Sauti Sol ambapo Rapper Diddy akiwa muandaaji mkuu wa Album hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *