Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Malaika amesema wakati anaanza muziki alikutana na changamoto ambayo ilimfanya kumaliza mwaka mzima bila ya kufanya mazungumzo na baba yake ambaye alikuwa anaamini muziki ni uhuni.

Malaika amefunguka hilo kutokana na sababu zinazofanya wasanii wa kike kuwa wachache kwenye kiwanda cha Bongo Fleva.

Amesema kuwa “Mimi wakati naanza muziki nilimaliza mwaka mzima bila mazungumzo na baba yangu kisa alikuwa naona kama uhuni, pili kumsimamamia msanii wa kike ni kazi kuliko mwanaume kwa sababu tunagharama nyingi ndio maana watoto wakike wanakuwa wachache kwenye muziki”.

Aidha Malaika ameendelea kusema “Tuna dhana ambayo ipo tangu zamani japo sasa hivi tunapambana nayo, iliaminishwa mtoto wa kike hawezi kufanya kitu na kipindi kile muziki ulikuwa ni wanaume wengi”.

Mwanamuziki huyo kwasasa ameupa kisigo muziki kutokana na kuwa bize na masuala yake mengine nje ya muziki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *