Muigizaji wa Bongo Movie, Auntie Ezekiel amesema kuwa kingine kinachoweza kuyafanya mapenzi yawe marefu ni kufahamu mipaka ya mwenzako na kutoingiliana.
Aunty Ezekiel ameyasema haya wakati alipofika Kids Fashion Empire ambako Mtoto wake na Kusah amepewa ubalozi wa duka hilo.
Pia amesema hajawahi kumuingilia Kusah kwenye ishu yake ya malezi na Mtoto wake na Ruby na hata Kusah mwenyewe huwa haingilii ya Auntie na Mzazi mwenzie Iyobo.
Muigizaji huyo amesema kuwa hana tatizo na mzazi mwenzake wala mzazi mwenza wa mpenzi wake wa sasa Kusah.