Msanii wa Bongo Fleva, Baba Levo amekanusha kuwa kauli yake haikumlenga Mwanamitindo na mjasiriamali, Hamisa Mobetto kama inavyotafsiriwa na baadhi ya watu mtandaoni na Hamisa mwenyewe.
Baba Levo alipangua madai hayo na malalamiko yaliyotafsiriwa kumlenga Hamisa kupitia video yake ambayo ilianza kusambazwa mitandaoni anayosikika akisema ‘Misa’ anaweza kujifungua ‘Mbwa’.
Baada ya kusambaa kwa video hiyo, Hamisa kupitia Insta Story alishusha lawama za moja kwa moja kwa msanii huyo hitmaker wa wimbo Shusha akiwa na Diamond Platnumz akionesha kutopendezwa na kauli hiyo ya Baba Levo.
Hata hivyo muda mchache baada ya lawama za Hamisa, Baba Levo kupitia akunti yake ya Instagram alikanusha madai hayo na nakueleza kuwa hajamtaha Hamisa kama inavyotafsiriwa bali alisema ‘Misa’.