Sehemu ya pili ya filamu ya Eddie Murphy ya Coming to America imeanza kuoneshwa Nigeria, Afrika Kusini na maeneo mengine duniani.

Filamu hiyo mpya inayoitwa ‘Coming 2 America’ imewahusisha waigizaji wakuu kama Murphy, James Earl Jones, Arsenio Hall, Shari Headley na John Amos.

Filamu hiyo iliyozinduliwa rasmi Marekani mwishoni mwa wiki, ina wahusika wengi kutoka Afrika wakiwemo wasanii maarufu.

Mwanamuziki maarufu wa Nigeria Davido ameshiriki katika filamu hiyo akionekana anatoa burudani. Wimbo wake wa ‘assurance’ndio aliuimba ndani ya filamu hiyo.

Msanii mwingine kutoka Afrika ambaye ameshiriki katika filamu hiyo kwa kuigiza ni Mnigeria anayefanya kazi Marekani Rotimi (jina lake kamili Olurotimi Akinosho)ambaye hivi karibuni amepata umaarufu mkubwa nchini Tanzania baada ya kuwa mchumba wa mwanamuziki Vanessa Mdee.

Nomzamo Mbatha, ni msanii kutoka Afrika Kusini anayeonekana katika tamthilia ya Isibaya.

Vilevile yupo muigizaji na mchekeshaji mwenye asili ya Ghana/Liberia- Michael Blackson (jina lake asili likiwa Jafari Ferguson). Ameweka sehemu ya picha ya filamu hiyo katika ukurasa yake ya Twitter; picha akiwa amevalia nguo za kijeshi.

Filamu hiyo ambayo imeangazia utamaduni wa Afrika haswa katika mavazi na mazingira yake, midundo na muziki wa Afrika.

Vilevile kuna mpango wa kuzindua mradi wa kurekodi ‘miondoko ya Zamunda’ unaojumuisha muziki kutoka Afrika kuanzia Mashariki ,Magharibi na Kusini mwa Afrika.

Wanamuziki kama Tiwa Savage naTekno, DJ Arafat from kutoka Côte d’Ivoire, Prince Kaybee na Msaki Afrika kusini, na Fally Ipupa kutoka DRC na Locko kutoka Cameroon.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *