Mwanamuziki mkongwe wa hip hop Bongo, Frofesa Jay amefunguka kuwa hafurahishwi na kinachoendelea kwa Young Lunya na Conboi.
Professor Jay amesema ni mapema sana kwao kuanza kuchukiana kwa sababu ndio kwanza safari yao ya muziki imeanza.
“Salama nikwambie ukweli kabisa kutoka chini ya uvungu wa moyo, kinachonikwaza katika game ya sasa hivi ni jinsi ambavyo watu hawapendani, hawachukuliani madhaifu ya mtu mwingine.
Mfano mimi na wewe tuko kundi moja, Mimi nika hit ila tuko kundi moja halafu wewe ukawa bado unasikilizia labda watu wamependa tu sauti yangu. Ukimuacha mwingine huwa inakuwa shida ni lazima wote tubebane.” alisema Prof na kuendelea
–
Mimi ni big fan wa Young Lunya na hata yeye mwenyewe anajua kabisa na nilishawahi kumwambia. Lakini sasa hivi unasikia kwamba kuna shida kati yake na Con Boi.
Ukisikiliza stori yao huwezi kuisikia pamoja, kuna kitu unakiona. Sasa mbona mapema sana? yani mapema sana kuanza kuona hawa vijana.
Yani sasa hivi ndio umeona tobo hili mwanangu mnaanza kupishana”!! alizungumza kwa uchungu Professor Jay akitolea mfano wa kundi lake la HBC walivyoshikana na kushindana wao ndani ya kundi bila kugombana na kupata mafanikio makubwa.