Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Mimi Mars amefunguka na kusema kuwa dada yake Vanessa Mdeee ambaye ni mwanamuziki wa Bongo Fleva hawezi kurudi Tanzania kwasasa.

Vanessa Mdee kwasasa anaishi nchini Marekani na mpenzi wake Rotimi hivyo kurejea huku kwa kipindi hiki itakuwa ngumu sana kwa mwanamuziki huyo ambaye aliamua kuachana na fani hiyo.

Mimi Mars amesema anam-miss dada yake Vanessa Mdee japo wanawasiliana kila siku kwa njia ya kupigiana simu na message.

Pia Mimi Mars amesema kuwa  “Tunamisiana sana lakini tunaongea kila siku kwa kupigiana simu na kutumiana message wala hatuna tabu hata kama yupo kule lakini bado yeye Mdee Music na anaendelea kusimamia harakati na michongo ya kwangu na ananishauri vitu mbalimbali ili tuzidi kutoboa”.

Vanessa Mdee anaishi nchini Marekani baada ya kuanzisha mahusiano na msanii wa filamu na muziki nchini Marekani ambaye ana asili ya Taifa la Nigeria Rotimi ambapo kabla ya hapo alikuwa na Juma Jux.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *