Umoja wa Mataifa umesema Makamu wa Rais wa zamani wa Sudan Kusini, Riek Machar ambaye alikuwa haonekana hadharani yuko nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Kikosi cha Majeshi ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa yaliyopo Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yalimsaidia yeye, mke wake pamoja na wengine kutoka kwenye mpaka unaogawa nchi hizo mbili.

Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir alimtimua kaz Machar baada ya mapigano baina ya majeshi yanayowaunga mkono na kusababisha maafa.

Machar aliondoka Sudan Kusini kwa kuhofia usalama wake ikiwa ni siku chache baada ya kuzuka mapigano kati ya vikosi vyake na vile vinavyoitii serikali ya Juba.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa, Farah Haq amesema Umoja wa Mataifa unatambua kuwa bwana Machar aliingia nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo kupitia mpaka baina ya Sudan Kusini na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo na kusaidiwa na majeshi ya Umoja wa Mataifa ya kulinda amani ambayo baadae walimsafirisha kwa ndege hadi mji mkuu Kinshasa.

Awali msemaji wa Riek Machar amesema Machar aliingia nchini DR Congo lakini alikuwa na lengo la kuelekea Ethiopia.

Machar anataka majeshi yasioyoegemea upande wowote yatumwe nchini Sudan Kusini ili kuhakikishiwa usalama wake baada ya walinzi wake na walinzi wa Rais Salva Kiir kupigana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *