Baada ya Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmonize kushuhudia mafanikio ya nyimbo zake alizoimba kwa lugha ya kingereza “Bedroom” na “Falling In Love” amewashauri wasanii kutumia lugha ya kingereza kwenye nyimbo zao lengo ikiwa ni kuutangaza muziki wetu na nchi yetu kwa ujumla.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika “Nina wajibu Wa Kuwashukuru Sana waanzirishi Wa Muziki Huu Ambao Leo Umekuwa Ajira Kwetu Naku Saidia Familia Zetu Nyingi Za Kimaskini Lakini Pia Wadau Na Mashabiki.

Kwaku Pambana Mpaka Tasnia Ilipofikia Hapa. Kiukweli Haikuwa Rahisi Lakini Pia Niseme Sanaa Yetu Imekuwa Kubwa Mataifa Kibao Wana fwata Tunacho Fanya ishara Tosha Kwamba Tunapiga Bao Ila Nika Kaujumbe Mfupi tuu Nadhani Ni Time Sasa Ya Kuutangaza Muziki Pamoja na Tanzania Mbali Zaidi Tumekuwa Tukiitangaza Rugha Yetu Pendwa Muda Mwingi Mno Na Kuifanya Imekuwa Rugha Maarufu Sana Africa.

KISWAHILI But nadhani ni Wakati Muafaka Wa Kuutangaza Muziki Wetu Pamoja Na Nchi Yetu…!!!! Zaidi Na Njia Rahisi Ni Kuimba Muziki wa Kitanzania naku Shoot Video Tanzania Ila Wimbo Unaimba kwa Rugha Ambayo Dunia Nzima Inaelewa.

Nayo ni (ENGLISH) Ndugu Wasanii Msiwe na Wasi Tuondoeni zile Zana Za Zamani Eti ukiiimba Kizungu Ngoma Haiwezi (HIT) Watanzania Wa Leo Sio Wajana Karibia Wote Wanatema (MAYAI) Mmeona Mifano Kama Bedroom na Failing in Love Hizi Zote ni (HIIIIT) Na Zimeimwa (ENGLISH) Japokuwa Ukitia Vineno Viwili Vitatu Vya Rugha Yetu Mama SIO MBAYA…..!!!! OK let’s Go KAKA ZANGU DADA ZANGU it’s time 4 Tanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *