Wasanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz na Nandy wametajwa kwenye orodha ya watakaoiwakilisha Tanzania kwenye Tamasha jipya la muziki, Sanaa na utamaduni litakalofanyika mjini Cancun nchini Mexico.
Diamond na Nandy wajumuishwa katika orodha ya utanglizi wa kati ya wasanii 10 watakaoshiriki tamasha hilo litakalifanyika kwa siku nne, kuanzia Septemba 2 hadi Sepetemba 6 katika viwanja vya ‘Moon Palace Resort’.
Wasanii wengine watakoshiriki tamasha hilo ni pamoja na Burna Boy, Roody Roodboy, Dexta Daps, Mr. Killa, Olatunji, Spice, Fireboy DML na King Promise.
Baada ya kutaja orodha hiyo waandaaji wa tamasha hilo wamesema kuwa wataendelea kutaja wasanii wengine watakaoshiriki tamasha hilo.