Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Lulu Diva amefunguka na kusema kuwa ni kweli mama yake anaumwa lakini hiyo haimfanyi yeye kutojiweka vizuri.
Lulu Diva alisema kuwa kuna baadhi ya watu wanataka awe mchafu eti kwa sababu tu mama yake yupo nyumbani ni mgonjwa jambo ambalo sio sawa.
Amesema kuwa “Kitu ambacho watu wengi hawakijui ni kwamba mimi natafuta pesa kwa ajili ya mama yangu, ili aweze kutibiwa vizuri, kula vizuri na kuishi sehemu nzuri.
Pia amesema kuwa anatamani siku moja mama yangu aweze kukaa na kuzungumza chochote na mimi kwa sababu sasa hivi ni mtu wa kukaa tu nyumbani, lakini hiyo hainizuii mimi kutovaa vizuri,”.