Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Rayvanny kutokea lebo ya WCB ameashiria album yake ya kwanza ‘Sound from Africa’ kuwa iko ukingoni kukamilika.

Rayvanny aliashiria hatua hiyo ya kukamilika kwa album yake ijayo, kwa mujibu wa ujumbe wake aliouweka kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Rayvany alitoa taarifa kuwa album hiyo ijayo kwa sasa imefikia 99% kukamilika ingawa hakuweka wazi ni lini rasmi album hiyo itaigia sokoni.

Hata hivyo bado haijabainika kama album hiyo itatoka chini ya lebo ya WCB Wasafi au itatoka chini ya utambulisho wa lebo yake mwenyewe, ambayo ilishathibitishwa kuwa pia ni miongoni mwa hatua na mipango yake ya baadae.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *