Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Alikiba amesema alishaachana na Lebo ya Sony Music baada ya mkataba wake kumalizika na sasa anafanya kazi na Kings Music pekee anayoimiliki mwenyewe.

Alikiba amesema Sony wanataratibu zao hasa upande wa utaoaji nyimbo kitu ambacho yeye binafsi anaona hakiendani na mazingira ya muziki wa Afrika.

Pia alisema ameachana na RockStar Africa ambayo kwa sasa inamsimamia Ommy Dimpoz pekee na hana tatizo na uongozi wa management hiyo.

Alikiba sio msanii wa kwanza kuondoka kwenye lebo hiyo ya RockStar Africa, kuna Lady Jaydee na Baracka The Prince nao walifanya kazi na lebo hiyo lakini wakaja kuachana na kila mtu anafanya kazi na kampuni nyingine.

Alikiba kwasasa ana milika lebo yake mwenyewe inayokwenda kwa jina la Kings Music inayowasamamia wasanii watata ambao ni K2ga, Tommy Flavour pamoja na Abdu Kiba ambaye ni mdogo wa Alikiba.

Alikiba kwasasa anatamba na wimbo wake unaokwenda kwa jina la Infedele ambao umepokelewa vizuri na baadhi ya mashabiki wa msanii huyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *