Aliyekuwa mke wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmonize, Sarah ametoa ujumbe ambao umetafsiriwa kama kijembe kwa mumewe huyo wa zamani.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Sarah anasema kuna baadhi ya wanawake hawana mbadala kabisa, ukiachana nae huwezi kumpata kama yeye.
“No lie, some woman are irrepleceable like the things she do for you and the feelings she had and showed you, you may never experience it again,” ameandika Sarah.
Harmonize na Sarah walifunga ndoa Septemba 2019 jijini Dar es Salaam, wanaripotiwa kuachana Desemba mwaka jana baada ya mwimbaji huyo kuweka wazi kuwa ana mtoto aliyempata nje ya ndoa.