Staa wa muziki wa Bongo Fleva, Rayvanny amefunguka na kuweza kwa mara ya kwanza kuwa anatarajia kuachia albam mpya mwaka itakapomalika.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Rayvanny amedokeza juu ya ujio wa Album yake ya ‘Sound From Africa’ ambayo huenda ikaachiwa Hivi karibuni baada ya kukamilika.
Sound From Africa itakuwa Album ya kwanza kutoka kwa Rayvanny toka aanze music ukiachana na EP yake ya Flowers aliyoiachia Mwezi Februari, 2020.
Mwanamuziki huyo amejizolea umaarufu toka asainiwe na lebo ya WCB chini ya Diamond Platnumz hivyo anataka kuachia albam yake ya kwanza kama msanii mahiri wa Tanzania.