Mwanamuziki wa Kenya, Tanasha Donna amewatoa udenda baadhi ya wanaume wakware ambao wamejikuta wakijiongezea machungu ya mwezi dume wa Januari.

 

Tanasha ambaye ni mzazi mwenza Diamond Platnumz ametupia picha yenye hapetaiti kwa wanaume katika kurasa zake za mitandao ya kijamii za Facebook, Instagram na Twitter.

 

Picha hiyo inamuonesha Tanasha akiwa ameinama na kubinuka kiasi cha kulionesha sawia lile umbo lake kwa nyuma akiwa amevaa kigauni chepesi cha zambarau na bluu, kiasi cha kumchora dhahiri shahiri namna ambavyo nguo ya ndani imemkaa.

 

“Hii ndiyo maana halisi ya mwanamke tajiri…” Aliandika Tanasha kusindikiza picha hiyo tamu.Walichokifanya wanaume hao ni kummwagia sifa kuwa ni mwanamke mzuri huku wakimuomba awajibu DM zao kwenye Instagram.

 

Mbali na hilo, baadhi ya mashabiki wake walimuita Diamond kutembelea kurasa hizo ili kumuona Tanasha alivyonoga ambapo itamlazimu sasa hivi kurejesha majeshi kwake.

 

Hata hivyo, Tanasha ameendelea kuuchuna bila kuwajibu chochote. Tayari Tanasha aliyetengana na Mondi mwanzoni mwa mwaka jana amekuwa staa mkubwa wa muziki wa Afrika Mashariki.

 

Ameanza mwaka huu wa 2021 vizuri kwa kuachia wimbo wake wa Kalypso ambao tayari umeanza kuweka rekodi Afrika Mashariki ukiwa na zaidi ya watazamaji laki 7 pale mjini YouTube ukishika nafasi za juu kabisa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *