Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Alikiba amesema kuwa ishu ya kutoa album kwa mwaka huu ipo kwa asilimia zaidi ya 100 na watu watarajie kuipata kabla haijafika mwezi wa sita.

Kiba alisema imepita miaka zaidi ya 10 tangu alipotoa albam ya Alikiba For Real, hivyo anaona ni wakati sahihi sasa wa kukata kiu ya mashabiki wake waliosubiri kwa muda mrefu sasa.

Huku akiongeza kuwa maandalizi kuelekea kwenye jambo hilo yapo vizuri zaidi hivyo mashabiki wake wakae mkao wa kula kuipokea albam hiyo.

“Watu wamesubiri albam yangu kwa zaidi ya miaka 10, nafikiri sasa ni wakati sahihi wa kufanya jambo kwa watu wangu wa nguvu. Haitafika hata mwezi wa sita mzigo utakuwa sokoni.”

Kiba ambaye anamiliki album mbili, Cinderella ya mwaka 2007 na Alikiba For Real iliyotoka 2009, kwa sasa anatarajia kuachia albam ya tatu toka aanze muziki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *