Tamasha la Muziki na Sanaa (Serengeti Music Festival) limeanza kwa kishindo na kuhudhuliwa na watu mbali mbali jijini Dar es Salaam.

Msanii mkongwe wa Bongo Fleva, Insspector Haroun amesema kuwa wasanii wa Tanzania wamepata kile walichokitafuta kwa siku nyingi.

Wasanii wa Bongo Fleva walionesha uwezo wao kwenye tamasha hilo lenye malengo ya kuunganisha utalii na sanaa, limeanza na limeweka viwango.

Kivutio kikubwa alikuwa mkongwe DJ Bon Love alirejea kwenye mashine ya one-on-two kuwachezesha wasanii wa zamani.

Mamia ya mashabiki waliojitokeza Uwanja wa Uhuru na maelefu zaidi waliofuatilia live kwenye tv na mitandaoni, waliposhangazwa kusikia muziki mzuri kutoka kwa wasanii walioonekana wameshapotea katika anga la muziki kama Wagosi wa Kaya, Z Anto, MB Dogg na wengine.

Mashabiki walipata show kali kutoka kwa wakali kama Baby Madaha, Wylumva Mmarekani mwenye asili ya Tanzania kutoka New York, TID, THT, Gozbert Goodluck, Chid Benz na Weusi.

Pia Tamasha la Serengeti linaendelea jana mjini Bagamoyo, Pwani, ambako litaungana na Tamasha la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni kuanzia saa 12 jioni ambapo pamoja na ngoma na sanaa zingine pia wakali kadhaa wa muziki wa kizazi kipya kutoka Dar es Salaam na kwingineko wataperform.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *