Aliyekuwa meneja wa msanii wa Bongo Fleva, Alikiba aitwae Seven Mosha ameteuliwa na kampuni ya Sony Music Africa kusimamia Masoko na Maendeleo ya wasanii katika Ukanda wa Afrika Mashariki.
Mosha ambaye ni Mkurugenzi wa RockStar Africa, atakuwa na jukumu la kuijenga kampuni hiyo ikiwemo kukuza wasanii wa Afrika Mashariki na kuwafanya wafanye vizuri ndani na hasa katika soko la kimataifa.
Mosha ambaye pia ni Meneja wa msanii Ommy Dimpoz atakuwa anaripoti moja kwa moja kwa mkurugenzi mtendaji wa Sony Music Afrika, Sean Watson.
“Seven ametumia karibu maisha yake yote kutoa mchango kwenye Muziki wa Afrika, ana passion na anafaa kuutangaza Muziki wa Afrika Mashariki kwenye Ramani ya Dunia”amesema Sean Watson
Haatua hii ya kuteuliwa kwa Mosha inakuja baada ya hivi karibuni Msanii Ommy Dimpoz kutangaza rasmi kuwa ameingia Mkataba wa ushirikiano wa kibiashara na Sony Music Entertainment Africa.