Mpenzi wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Rayvanny aitwae Fayma amefunguka na kusema kuwa hana tatizo na mzazi mwenzake huyo licha ya maneno kuwa mengi mtandaoni.
Fahyma amesema kuwa, hayupo tayari kumuacha mumewe huyo kwani wametoka mbali sana katika mahusiano yao ya kimapenzi.
Fahyma ambaye ni mwanamitindo maarufu Bongo amesema kuwa, aliacha kunyonya ziwa la mama yake, lakini siyo rahisi kuachana na Rayvanny hivyo wataendelea kuwa kwenye mahusiano kama kawaida.
Pia amesema kuwa Kuna watu wanatamani mimi na Rayvanny tuachane, lakini hilo haliwezekani kwa sababu binafsi nilifanikiwa kuacha ziwa la mama yangu, lakini siyo kumuacha mume wangu.
Wawili hao wamejaaliwa kupata mtoto mmoja wa kiume aitwaye Jaydenny baada ya penzi la wawili hao kudumu kwa muda mrefu.