Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ommy Dimpoz amesaini mkataba wa ushirikiano kibiashara na kampuni maarufu ya muziki, Sony Music Africa yenye makao yake makuu mjini Johannesburg nchini Afrika Kusini.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Dimpoz alithibitisha hilo na kutangaza rasmi kuwa wimbo wake wa kwanza ‘Dede’ kutoka kwenye album yake ijayo utatoka rasmi jioni ya Desemba 10 2020.
Wimbo huo mpya kutoka kwa Ommy Dimpoz, umewashirikisha, Dj Tira, Dladla Mshunqisi na Prince Bulo.
Dimpoz pia aliweka wazi kuwa album yake hiyo inayosubiriwa kwa hamu kubwa itatoka rasmi mapema Mwakani(2021) ikiaminika kuwa itatoka rasmi chini ya ushirikiano wake na ‘Sony Music Africa’.