Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Wini amesema licha ya wasanii wa kike kutongozwa na maproducer au directors pia wana gharama sana kwenye muziki kuliko wasanii wa kiume.

Wini amesema kuwa msanii wa kike anatakiwa apendeze kila wakati asipokuwa na menejmenti au sapoti itampa ugumu kushine ambapo akajitolea mfano kwa kusema aliwahi kununua nywele za gharama ya Milioni 1.

“Kwangu mimi kutongozwa sio changamoto kubwa kwa sababu sijaanza kutongozwa kwenye muziki ila najua jinsi ya kukabiliana na hiyo ishu.

Pia amesema kuwa kwenye muziki kuna changamoto nyingi kuliko za kutongozwa kwanza wasanii wa kike tuna gharama kuliko wasanii wa kiume,  kama anakuwa hana menejmenti au sapoti inakuwa ngumu kwake”.

Aidha msanii huyo ameendelea kusema “Vitu ni vingi kwa msanii wa kike anatakiwa apendeze kila wakati ila mimi napendaga kuwa ‘natural’, kitu cha gharama ambacho niliwahi kununua ni nywele zangu za milioni 1 na laki 2”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *