Muigizaji wa Bongo Movie, Wema Sepetu amevunja ukimya na kusema kuwa siku Mungu akimjalia kupata mtoto wake lazima achanganyikiwe kwanza kwa furaha.

Wema ambaye kwa sasa anatamba na kipindi chake cha mapishi cha Cook With Wema Sepetu, ameeleza hilo kwenye Insta story yake baada ya kutoa nafasi ya kuulizwa maswali na mashabiki wake ambapo moja ya swali lilikuwa ni siku akipata mtoto itakuwaje ambapo alijibu.

“Nikipata mtoto wangu naweza nikachanganyikiwa siku mbili au tatu naamini, hata mimi ningependelea hivyo ipo siku inshaallah,” alijibu Wema.

Hata hivyo kuhusiana na kumualika Zari kwenye kipindi chake, Wema amesema kuwa kama Zari akiridhia, anaweza kumualika kwani yeye hana tatizo naye.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *