Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewataka wakadiriaji majenzi nchini wahakikishe wanafanya kazi kwa kuzingatia maadili na waepuke vitendo vya rushwa.

 

Makamu wa rais ameyasema hayo wakati akifungua mkutano wa mwaka wa wakadiriaji majenzi kutoka nchi mbalimbali za Afrika jijini Dar es Salaam.

 

Pia amesisitiza kwa sasa serikali ipo kwenye mchakato wa kuanza kutekeleza miradi mikubwa ya kiuchumi ikiwemo ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa na ujenzi wa bomba la mafuta kutoka nchini Uganda hadi Tanga.

 

Makamo wa rais amesema serikali inatambua mchango wa watalaamu wa ukadiriaji majenzi hivyo ni muhimu kwa wataalamu hao wakauongeza bidii katika utekelezaji wa kazi zao hasa kwa kuzingatia teknolojia za kisasa.

 

Pia amehimiza ushirikiano kati wakadiriaji majenzi wa Tanzania na wa nchi nyingine za Afrika katika kubadilishana uzoefu kwenye kazi zao ili kuongeza ubunifu na ufanisi katika miradi wanayopata.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *