Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Bill Nass amesema kuwa kuna changamoto alizokutana nazo ndio zilizopelekea kuchelewa kwa ndoa yake na mwanamuziki mwenzake Nandy.
Bill Nass ameeleza kuwa kuna changamoto alizokutana nazo ndio zimepelekea kuchelewa kwa ndoa yake na mrembo huyo wa Bongo Fleva.
Billnass amesema kuwa “Unapotaka kufanya jambo lolote kubwa zuri la kimaisha, lazima uzingatie vitu vingi ili kufanikisha suala hilo.
Kwa hiyo hatua kubwa naamini nimeshaifanya kuelekea hatua nyingine ni mimi, dua zenu zinahitajika. Si jambo rahisi na ukizingatia mwaka huu kulikuwa na vitu vingi Corona, ilikuja jambo la Uchaguzi na vitu vingine.
Pia ameongeza kwa kusema kuwa Na mimi pia nahitaji jambo langu la kihistoria ukizingatia harusi ni mara moja ndoa ni mara moja kwa sisi Wakristo na ukizingatia kuna vitu havikuwa sawa.” ameeleza Bill Nass.