Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Tommy Flavour amesema hataki kufananishwa na wasanii wengine ambao wapo kwenye lebo zingine kwa sababu kila mtu ana mikakati yake kwenye suala zima la kufanya kazi.
Kauli ya msanii huyo inakuja kufuatia mashabiki wa muziki nchini kumwambua kuwa anashindwa kuachia ngoma mfululizo kutokana na lebo yake ya Kings Music haina utaratibu huo kama ilivyo kwa lebo nyingine ambazo zinampromote msanii wao ili kufika mbali.
Tommy Flavour amesema promotions wanazofanyiwa wasanii wengine kwenye lebo zao wala hata hazimshuti ila anachoamini ni uwezo na kipaji cha mtu ndiyo kitamfanya awe juu kuliko kutumia nguvu ya promotions.
Amesema kuwa “Hata kama unam-promote vipi msanii ila uwezo na kipaji chake ndiyo kitambeba na ndiyo itamfanya aendelee kwenye muziki, mimi naamini nitafika mbali na menejmenti yangu itanifikishia hilo, hata walivyonisaini haikuwa kwa ajili ya kunishindinisha na wasanii wengine kutoka lebo zingine”.
Mwanamuziki huyo chini ya lebo ya Kings Music inayomilikiwa na Alikiba amefanikiwa kuachia nyimbo hadi sasa toka alipotambulishwa ndani ya lebo hiyo mapema mwaka huu.