Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Dully Sykes amesema alipata umaarufu kabla haijaingia mitandao ya kijamii ambayo kwa sasa ndiyo chachu ya kusaidia kuongeza umaarufu kwa wasanii wengi.
Dully Sykes ameeleza kuwa hakuna kitu kinachoweza kumpa mtu umaarufu tofauti na kuchapa kazi.
Dully amesema kuwa “Kuwa tajiri au masikini ni majaliwa ya Mungu, mimi nilipata umaarufu kabla ya Facebook, WhatsApp, Instagram na Twitter, kazi ndiyo inambeba msanii ili kufikia mafanikio.
Ameongeza kwa kusema kuwa hakuna mzembe anayefanikiwa hata ukitumia mitandao yote kama huna juhudi haina maana hata meneja huwa wanaangalia msanii anajitahidi vipi”.
Aidha msanii huyo ameongeza kuwa “Kuna watu wameumbwa kusaidia watu hata wakitendwa mimi nasaidia wala sisubiri fadhila kutoka kwa mtu, nasaidia mtu nikamaliza nafanya mambo yangu na yeye afanye yake”.