Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Linex amemtaka msanii Baba Levo kumuheshimu kufuatia kitendo cha kumpokea na kumsaidia kipindi alivyokuja Dar Es Salaam kutoka mkoani Kigoma.
Linex amesema kuwa wakati huo hata yeye alikuwa hana ghetto bali alimuombea kwa rafiki yake ili wakae pamoja jijini Dar es Salaam lakini anashangaa sasa hivi hataki kukumbuka wema aliomtendea badala yake anamsema vibaya.
“Hata ikitokea nimegombana na Baba Levo hakuna media wala mtu ambaye hataweza kuingilia ugomvi wetu, nilimpa imani kabla ya watu kumjua na hajaonekana niliamini kipaji chake.
Msanii huyo amesema kuwa kitendo cha mtu kukupa nafasi ukae kwenye ghetto hali ya kuwa yeye mwenyewe sio ghetto lake ni kutendo ambacho Baba Levo anatakiwa akiheshim miaka yake yote ya sanaa, kama akikichukulia poa atakuwa hayupo sawa.