Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Young Killer ammwagia sifa za kumkubali sana aliyekuwa mpenzi wake, mwanama kunako Bongo Movie, Jackiline Wolper.

Young Killer amesema kuwa Wolper ni mwanamke wa kitofauti sana kwani akipenda anapenda kweli kweli, na mbali na hilo pia ni mtafutaji.

“Wolper ni mwanamke mrembo, mbali na urembo pia anajua kupenda maana akikupenda anakupenda kwelikweli.

Pia amesema kuwa ni mtafutaji anapambana sana, bado naenelea kumkubali maana hatujaachana kwa ugomvi kivile adi tushindwe kuongea au kuendelea kuwasiliana,’.

Ikumbukwe Young Killer alikuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na muigizaji huyo wa Bongo Movie licha ya kuficha mahusiano yao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *