Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Shilole amekanusha kurudiana na mume wake baada ya video kusambaa mtandaoni wakiwa wote licha ya kupokea kupigwa na mwanaume huyo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Shilole ameibuka na kukanusha juu ya video inayo sambaa kwenye mitandao ya kijamii ikimuonesha akiwa na aliyekuwa mume wake Uchebe huku akisikika akisema kuwa wamerudiana

Shilole ameandika “Nimeona kuna taarifa nyingi zinatengenezwa, kuona uongo mwingi unapikwa kuhusu mimi na sakata la ndoa/kupigwa.

Pia ameendelea kuandia Kuna video inaasambazwa, tuko sisi na bwana mmoja anitwa Aristote. Ile video ni ya siku nyingi sana. Naomba muipuuze.

Amemalizia kuandika Suala langu lilihusisha vyombo vya dola/sheria. Hivyo sio jambo la kusema tu kwa sasa. Wakati unakuja (sio mbali), nitaeleza yote kwa utaratibu, na kwa undani”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *