Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmorapa ambaye ni bingwa wa mitandao amekataa kumuomba msamaha Harmonize baada ya kumblock katika mtandao wa kijamii.

Harmonize amesema kuwa suala hilo haliwezi kutokea kwani hakuna jambo ambalo amemkosea mpaka akaamua kumblock mtandaoni.

Pia Harmorapa amesema kuwa suala la kublokiwa na Harmonize lina stori ndefu na hawezi kulizungumzia kwa sasa ila ikifika muda ataweka wazi kila kitu.

Amesema kuwa “Siwezi kukaa kumuomba msamaha kwa sababu, sidhani kama kuna jambo nimemkosea, kwanza kila mtu ananyota yake na siwezi kutembelea nyota ya mtu.

Ameongeza kusema kuwa Mungu aliyeniumba mimi ndiyo kamuumba yeye na watu wote kwahiyo haiwezi kutokea kumuomba msamaha kisa nimetembelea nyota yake na sijamkosea kama ningemkosea ningemuomba msamaha, hata mimi nilikuwa na upepo wangu”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *