Mwanamuziki wa Hip Hop Bongo, Stamina amesema suala la kumuomba msamaha aliyekuwa mkewe ni jambo la siri na la watu wawili.

 

Stamina amesema haliwezi kuwa jambo la kuweka hadharani kwani wakati wanakubaliana kuwa kwenye uhusiano hakuwaambia watu.

 

Pia amesema kuwa “Mimi sijaweka uhusiano wangu wala kumuonesha mke wangu, ule ni muziki tu, halafu sijui kwa nini Watanzania hawaamini kwamba naweza nikamuimbia mtu mwingine.

 

Amemaliza kwa kusema kuwa “Masuala ya kuombana msamaha ni mambo binafsi ya watu wawili, kama yeye ameomba msamaha au mimi nimeomba msamaha ni vitu binafsi na hata ikitokea hivyo lazima ianze kwa watu wawili siwezi kuja kuvisema hadharani kwa watu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *