Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Shilole amefunguka na kukiri kuwa mumewe, Ashraf Uchebe amemtaka kufanya mazoezi ili kupunguza tumbo kutokana na kuwa mnene sana.
Shilole amesema kuwa mara nyingi Uchebe amekuwa akimsifia na kumwambia anazidi kuwa mzuri licha ya kuwa nje watu wanakesha kumwambia apungue, jambo ambalo haliafiki sana zaidi ya kumwambia apunguze tu tumbo.
“Nafanya sana mazoezi ya kupungua, lakini unene wangu siyo kero kwa mume wangu, tena ndiyo anazidi kunipenda.
Pia amesema kuwa mara nyingi anamwambia mwili wake mzuri ila hajitahidi kupunguza tumbo tu ila mwili upo vizuri.