Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Lulu Diva amefunguka na kusema kuwa kuwa yeye ni mwanamke mchapa kazi tofauti na watu wanavyomuona.

Lulu Diva amesema kuwa yeye ni binti anayejua wajibu wake na pia siyo mtu wa kutumia pesa hovyo kwenye starehe kama ilivyo kwa mastaa wengine.

Pia amesema anamshukuru mama yake kwa kumfundisha jinsi ya kupambana na maisha, lakini pia kujua lipi jema na lipi siyo jema.

Amesema “Mimi nikiwa na njaa, napika nyumbani kwangu, siyo kwenda kununua mahotelini. Hayo maisha mimi sina, ukiona nimefanya hivyo, ujue ni mara chache mno na kuwe na sababu,”.

Mwanamuziki huyo kwasasa anatamba na ngoma yake mpya iitwayo Come Again aliyomshirikisha Eddy Kenzo kutoka nchini Uganda.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *