Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Madee ameitetea timu yake ya Yanga baada ya kuchezea kichapo kutoka kwa KMC kwenye mchezo wa mechi ya kirafiki uliochezwa siku ya jana Juni 8, 2020.

Madee amesema Yanga imefocus sana kwenye ligi, wachezaji walikuwa wamekaa kwa kipindi kirefu ndani hadi wengine tumeambiwa wameongezeka uzito na hawajaweza kuwa sawa.

Pia amesema chochote kingeweza kutokea sio zile 3 wangeweza kufungwa hata 9, mchezo wa mpira wachezaji wasipocheza kwa pamoja kwa wiki mbili ni tatizo” ameeleza Madee.

Ameongeza kusema kuwa kwa sababu ni mechi ya kirafiki hakuna mtu anayeweza kukurukia kwenye miguu ili achukue mpira kwa sababu kuna michezo muhimu mingine.

Mwisho ameendelea kusema kuwa ila ikitokea kwenye game ya ligi kama tukifungwa tena nitaeleza vizuri”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *