Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Mwana FA amemkumbuka aliyekuwa mwanamuziki wa Bongo Fleva Albert Mangwer maarufu kama Ngwear ambaye aliaga dunia miaka saba iliyopita nchini Afrika Kusini.
Mwana FA kupitia ukurasa wake wa Instagram amemuelezea mwanamuziki ambaye alikuwa mtu wake wa karibu kipindi cha uhai wake.
Mwana FA ameanza kwa kuandika
Kitu kikubwa kuliko vyote kwangu kutoka kwenye sanaa ya Ngwea ilikuwa ni urahisi kwenye mziki wake. Alikuwa na uwezo wa kufanya mtu yeyote,wakiwemo wasio wapenzi wa hiphop/rap wafurahie anachokiwasilisha.
HAKUWA ANAIMBIA MARAPPER WENZAKE, ulikuwa ni mziki wa watu..na ndio maana nyimbo zilikuwa na uwezo wa kukatiza kwenye matabaka na rika zote bila wasiwasi na kila mtu akaweza kujinasabisha nao.
Miaka 7 baadae(toka utukatae) bado tunakula magoma yako kama yametoka tu jana mzee baba..so upo around mazee. Bado natabasamu kila nikiskia Ghetto Langu utasema ndio nalisikia mara ya kwanza, Rest Eazy Mazee. Ntakuandikia waraka mreeefu hivi karibuni nikuelezee tulipofikia”.